BOFYA HAPA>>>>KUJIUNGA KATIKA CHANNEL YETU YA TELEGRAM ILI KUPATA TAARIFA MPYA ZA ELIMU NA KAZI KILA SIKU(BURE)

HESLB TAARIFA MUHIMU: MASAHIHISHO YA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD MWANACHUO APP

Higher Education Students’ Loans Board (HESLB): The focus is on both issuance and recovery of loans from higher education loan beneficiaries. Over the past years, since its establishment in July 2005, the Board has managed to issue loans to needy students and the trend shows a steady growth.

[HESLB]TAARIFA MUHIMU: MASAHIHISHO YA MAOMBI YA MIKOPO 2019/2020

HESLB imeongeza muda wa siku mbili kwa waombaji mikopo kwa mwaka wa masomo 2019/2020 ambao fomu zao zilibainika kuwa na upungufu ili wakamilishe marekebisho hayo hadi Jumapili Oktoba 6, 2019 saa 5.59 usiku.
Nyongeza ya muda wa marekebisho inalenga kuwapatia fursa waombaji wanaotakiwa kufanyia marekebisho fomu zao za maombi na ambao kwa kufunga mfumo leo Oktoba 4, 2019 iliyokuwa tarehe ya mwisho kwa mujibu wa tangazo la Septemba 29, 2019; hawataweza kukamilisha.
Hadi kufikia leo Oktoba 4, 2019, kati ya wanafunzi 10,571 ambao fomu zao za maombi zilibainika kuwa na upungufu, waombaji 7,558 wamekamilisha kufanya marekebisho, idadi ambayo ni sawa na 71.6%. Idadi iliyobaki ya waombaji mikopo 3,013 (28.4%) ndio ambao hawajakamilisha masahihisho.
Hatua ya HESLB kuwaita baadhi ya waombaji mikopo kufanya masahihisho kwenye fomu zao inafuatia kukamilika kwa uhakiki wa maombi ya mikopo ambapo ilibainika baadhi ya fomu za maombi ya mikopo zina upungufu unaozuia kuendelea na hatua ya kupangiwa mikopo.

Upungufu huo ni pamoja na kukosa nyaraka ama viambatanisho vilivyothibitishwa na mamlaka husika na saini za waombaji na wadhamini wao.
 
Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shahada ya kwanza *bofya hapa.*
Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shule ya Sheria (Law School of Tanzania) *bofya hapa.*
Ili kuona orodha ya majina na marekebisho yanayohitajika kwa Shahada za Uzamili na Uzamivu*bofya hapa.*

SHERE

Leave a Reply

Your email address will not be published.

BOFYA HAPA KU DOWNLOAD MWANACHUO APP

%d bloggers like this: