Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

Je Raisi Magufuli anaweza kuvunja mikataba tata ya madini?

Ukisikiliza hotuba nyingi za raisi Magufuli tukianzia na ile ya mkutano wake na wazee wa dar es salaam, mkutano wa na engineers, na mkutano wake wa majuzi na waandishi wa habari amekuwa akiongea waziwazi bila kuficha jinsi anavyoumia na mikataba ya madini iliyosainiwa na watangulizi wake. Raisi anaona mikataba hii haikuwa na nia ya dhati kwa masirahi mapana ya taifa zaidi ya kutonyonya na kutuibia utajiri wetu. Sasa swali ni je Raisi Magufuli anao uwezo wa kuvunja hii mikataba hasi?

Comments

  • @tanzaniaone Raisi Magufuli sio anaweza tu kuvunja pia anaweza kufuta hizi kampuni kabisa kufanya uchimbaji hapa ila shida ipo kwenye malipo ya fidia yatakuwa makubwa sana, ila sio kwamba Raisi ameangalia tu kama waliopita, ameshaanza kutafuta haki yetu yote itokanayo na sheria ya uchimbaji wa madini, wachimbaji lazima wazifuate, mfano mzuri ni Tanzanite Raisi amejitahidi sana, sasa ata migodi midogomidogo ya wachina waliokuwa wanakwepa kodi inafungwa. Naamini Raisi Magufuli anafanya kila awezalo kuhakikisha mali yetu haiendi bure.
  • @Africaner asante kwa maelezo yako, ila sasa kama anaweza mbona ata hayo madongo ameshindwa kuyazuia kutosafirishwa maana amekuwa akisema ana mashaka na huo mchanga kama hauna madini.
  • @tanzaniaone hili jambo si rahisi kama unavyozania, jua kabisa makosa yalifanywa na wale waliosaini hii mikataba, hawakuwa na uzalendo na inchi yetu. Kama nilivyokwisha kusema Raisi Magufuli ni mzalendo tena yule aliyeiva, hana mchezo kabisa, nakuhakikishia utajionea mwenyewe atavyopata njia ya kuwakamata hawa wachimbaji, naamini Raisi halali juu ya hali hii sasa its a matter of time you will see. Cha kwanza hakuna tena tax holiday za kijinga makampuni yalikuwa hayalipi kodi kila muda wa kulipa ukifika yanabadirisha majina, sasa hakuna tena huo upuuzi trust me we have a great leader, Magufuli is the best president after Nyerere.
Sign In or Register to comment.