Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

Ahadi ya pensheni kwa wazee itekelezwe


Serikali iliahidi kuanza kuwalipa wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 pensheni ya 45,000 kuanzia mwaka wa fedha 2011/2012. Vyombo vingi vya habari likiwamo mwanainchi la january 5, 2011 vilitangaza. Aliyekuwa waziri mkuu, Mizengo Pinda alitoa ahadi hiyo alipokuwa akizungumza na wazee wa mkoani katavi. Wazee tulifurahishwa na mpango huo wenye matumaini ya maisha bora. Kwa kuwa hapakuwa na maelekezo ya atakayewalipa, kuanzia Agosti walianza kwenda ofisi mbalimbali kuuliza wakianza za kijiji. Kata wilaya mpaka mkoa na kote hakukuwa na taarifa za malipo hayo. Baadae aliyekuwa waziri wa kazi na ajira Gaudensi Kabaka akasema wazee hao wangeanza kulipwa kuanzia mwaka wa fedha wa 2013/2014 cha kushangaza, Naibu waziri wa fedha na mipango, Ashatu Kijaji ametangaza penseni hizo zitaanza kulipwa mwaka huu wa fedha wa 2016/2017 lakini mpaka sasa (Oktoba) hakuna ofisi ya umma yenye taarifa hiyo. Jamani serikali hebu walipeni wazee wetu, sie wanafunzi wa chuo tumekubali hekaheka ya ahadi ya mikopo ambayo kwa kiasi kikubwa haikizi mategemeo tuliyokuwa nayo.

Comments

  • Kwakweli ni jambo la kuhuzunisha, ila subira yavuta kheri naamini serikali itaanza kuwasaidia wazee wetu.
  • Shida ni madeni makubwa ya awamu ya nne iliyoyaacha, kingine walikuwa wakitoa ahadi wakijua hawatazitekeleza, kumbuka kampeni za uchaguzi mwaka 2010, waliahidi mengi kuwaamanisha wanainchi wawachague ilihali haikuwa kweli, kabla ya uchaguzi walipitisha mambo mengi bila kuyafanyia tathmini ya kutosha wenyewe walilenga tu kushinda uchaguzi sasa awamu ya tano ndio inabeba zigo lote na hili la pension likiwamo.
Sign In or Register to comment.