Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

Kama wanafunzi tumelipa ada walimu kutoingia darasani vyuoni je ni uvivu au mgomo baridi wa malipo?

Jamani kuna vyuo nikianza kuviorodhesha hapa Tanzania nitaleta tafurani, uongozi wake ni hodari mno kwenye kudai ada lakini walimu wavivu kutekeleza majukumu yao.
Utakuta chuo, hakikubali kukupokea mwanafunzi hadi upeleke karatasi ya malipo ya ada yao tena ikiwa imekamilika. Hakuna anayekusikiliza pale unapokwenda kuomba ili angalau wakupe muda wakati jitihada za kuipata inafanyika. Lakini kwa upande wao sasa ukiwa umelipa ada ili kuanza masomo, utasikia mara leo sijui nani hayupo, mara leo masomo yatakuwa hivi, mara hiki hakuna. Kama ambavyo wanakuwa hodari wa kudai ada, wangekuwa hivyo hivyo kwenye kutekeleza wajibu wao wa kutoa elimu iliyokusudiwa kwa kiwango kilekile bila shaka elimu ya Tanzania ingekuwa bora na wanafunzi husika wangepata walichokitarajia.
Sign In or Register to comment.