Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

Korosho bei juu, wakulima kero tele


Baadhi ya wakulima wa korosho wilayani Masasi wamedai kutolipwa licha ya kufanyika minada minne ya mauzo ya zao hilo na tena kwa bei ya juu. Wakulima walitoa madai yao mbele ya mkutano wa hadhara na Mbunge wa Ndanda, Cecil Mwambe kwenye kata ya Mlingula. Wanadai licha ya uwapo wa bei nzuri ya korosho bado hawajalipwa. Mbunge Mwambe alisema kwa utaratibu walipaswa kulipwa ndani ya siku tano lakini wamecheleweshewa malipo, hivyo aliahidi kulifanyia kazi suala hilo. Wakati huohuo, wakulima hao walishauri serikali kuwekeza kiwanda cha juisi au pombe itokanayo na mabibo ili kuwaongezea kipato.
Sign In or Register to comment.