Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

In this Discussion

Miaka 12 ya bodi ya mikopo, kero zilezile.

Nakumbuka zaidi ya miaka 10 iliyopita wakati bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) ilipokuwa ikianzishwa. Yalikuwa ni mabadiliko ya mataifa mengi duniani.
Mahitaji ya kiuchumi yalizifanya serikali nyingi kubadili mfumo wa ufadhili wa elimu hii ambayo kabla ya hapo ilikuwa ikitolewa bure. Julai 2005 bodi hii ilianza kutoa huduma katikati ya changamoto kibao.
Kuna mambo mawili yaliyotokea mwaka huo. Mabadiliko ya kisera. Kwanza ilikuwa udahili na pili ni huo ufadhili.
Kabla ya mwaka wa masomo 2005/2006 wahitimu wa kidato cha sita walikuwa wanalazimika kukaa nyumbani kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu kabla ya kujiunga na chuo kikuu.
Mihula yao ilikuwa inaisha Juni ila walikuwa wanajiunga chuo mwishoni mwa Oktoba au mwanzoni mwa Novemba kama ilivyo sasa.
Lakini mwaka 2005 mabadiliko yalifanyika muda wa masomo ya kidato cha sita ulipunguzwa kwa miezi mitatu. Walimaliza Machi badala ya Juni na wakaruhusiwa kujiunga nachuo mwaka huo huo. Ni utaratibu unaoendelea mpaka sasa.
Nakumbuka kulikuwa na in-take mbili kwa wakati mmoja. Wahitimu wa mwaka 2004 na wale wa 2005 wote walikuwa wakigombea nafasi zilezie za vyuo vichache vilivyokuwapo wakati huo. Wachache walichukuliwa, wengi waliachwa.
Wanafunzi walikuwa wengi kuliko uwezo wa vyuo. Wale waliobahatika kujiunga walikutana na changamoto ya mikopo kutoka bodi. Kila kilichokuwa kinaelezwa kilikuwa kigeni. wanafunzi walijikuta hawaelewi, wazazi na walezi pia.
Wanafunzi wakawa hawana budi zaidi ya kuingia barabarani, wakaandamana kushinikiza wapewe haki yao, hali hio haikushangaza sana kwasababu ilijitokeza kwenye mataifa mengi.
Wavumilivu waliamini hiyo ni hali ya mpito tu kadri ya muda unavyozidi kwenda mambo yatatengamaa. Wakaipa bodi muda ile ijipange na kusawazisha sehemu zisizo na udhoefu ila mpaka sasa hilo halijafanikiwa bado.
Yapo mambo mengi ambayo hayaendi sawa mpaka leo miaka 12 tangu kuanzishwa kwake wapo wanafunzi wanaopitia waliyoyapitia kaka na dada zao.
Wanafunzi hawana uhakika wa mikopo, wakikosa wanafanya kingine nje ya mipango waliyojiwekea. Kuonyesha kulemewa masharti yameongezeka, makundi ya wasiostahili yanaongezwa, ata iliwahi kutolewa kauli tata kuwa wafanyakazi wasikopeshwe bila kuangalia wana mishahara kiasi kipi, jambo hili linawezekana kweli inchini?
Taasisi nyingi za mikopo huwa zinatafuta wateja lakini bodi hii imelemewa nao, hakuna anaekuja na wazo mbadala la kuongeza mtaji kukidhi mahitaji. Wanafunzi wengi wanakosa mikopo hata wanaobahatika kupata wanapewa kwa asilimia kadhaa. Bodi bado inajipanga.
Kukosa au kupewa sehemu ya gharama zinazohusika ni moja ya changamoto ambazo bodi hii bado haijafanikiwa kuziondoa. Mfano ni wachache sana tena wanaofundisha Vyuo vikuu ndiyo wanaweza kupata mikopo kwa shahada za uzamili na uzamivu.
Changamoto kubwa kuliko zote ni ukusanyi wa mikopo iliyotolewa. Bodi haina taarifa kamili kuhusu waliokopeshwa, ndio maana inahangaika bila mafanikio makubwa. Haitambui nani yupo wapi; yupo hai ama kafariki; kaajiliwa au kajiajiri n.k.
Kwenye orodha ya wadaiwa sugu iliyotolewa kuna majina ya wengine ambao hawajawahi kukopa ama waliomaliza kulipa, hivyo bodi ya mikopo bado ina kazi kubwa kupata matokeo chanya ya malengo ya kuanzishwa kwake.
Imeandikwa na Julius Mathias.

Comments

Sign In or Register to comment.