Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

Wanachuo Dodoma wadaiwa kujiuza kwa Kutumia Picha.


Mtandao wa Wanawake Tanzania(Afnet), umetoa repoti polisi ukidai kuna udalali wa biashara ya ngono kwa wanafunzi wa vyuo kadhaa vya Dodoma unaofanywa na mameneja wa hoteli zilizopo katikati ya mji.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Afnet, Sara Mwaga alipokuwa akizungumza kuhusu maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa Kanda ya kati ambayo kaulimbiu yake ni 'Funguka chukua hatua, mlinde mtoto apate elimu'. "Tumepata taarifa ziko baadhi ya hoteli hapa mjini ambazo watoto wetu wa vyuo wamepeleka picha zao kwa mameneja anapokuja mteja anahitaji huduma ya msichana anaonyeshwa zile picha", alisema na kuongeza: " Akichagua anapigiwa simu kama yupo wapi anapanda bodaboda ndani ya dakika 10 au 20 anamhudumia mteja anarudi".
Alisema hayo mbele ya Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Ernest Kimola na maofisa wengine wa jeshi hilo na wawakilishi wa Mtandao wa Kupambana na Ukatili wa Kijinsia(Mkuki). "Vijana wa chuoni wako katika mazingira hatarishi kwani wengi wao huenda shule wakiwa hawana fedha kutokana na umaskini wa familia zao. Sasa inapocheleweshwa au kutopatikana kabisa huwaweka katika mazingira hatarishi ya kushawishiwa kimapenzi", alisema. Alisema hali hiyo inawafanya wengine kufikia hatua ya kuuza miili yao ili wapate fedha na vitu vingine.
Sign In or Register to comment.