Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

NMB YATOA MSAADA WA KOMPYUTA 250 KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI NCHINI

Benki ya NMB imeendelea kusaidia kukuza elimu nchini kwa kutoa msaada wa kompyuta 250 ambazo zitagawiwa kwa shule za msingi na sekondari nchini ikiwa ni siku sita tangu ilipotoa msaada wa madawati 3,500 kwa shule 71 nchini.

Akizungumza wakati wa halfa ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker alisema msaada huo ni sehemu ya mpango ambao NMB imeuweka wa kusaidia jamii (CSR) na kupitia msaada huo wanaamini utaweza kukuza elimu katika masomo ya Tehama.
Sign In or Register to comment.