Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

In this Discussion

USIMAMIZI WA MITIHANI KWA BAADHI YA VYUO NI MBOVU SANA

Mtihani si jambo la mzaha, katika kutengeneza nguvu kazi ya taifa, ikumbukwe kuwa ni matokeo ya mitihani ndio huangaliwa kama kigezo cha ubora na ufanisi wa mtu fulani, pale anapoomba ajira au mkataba wa aina yoyote ile. Sasa basi, wanafunzi wengi wamekuwa wakiiba mitihani, na mbaya zaidi nimewahi kushuhudia kwa macho yangu, wanafunzi wakiingia na smart phones kwenye vyumba vya mitihani, yaani wamebeba notice zote, na watatumia smart phones zao kuangalia majibu bila kushikwa. Sasa najiuliza wasimamizi wanakuwa wamelala? Utaona wasimamizi wanajifanya wakali kweli, ila wanashindwa kabisa kuwashika wezi wa mitihani. Matokeo yanapotoka mtu ambaye haudhulii vipindi kama inavyotakiwa, anayelipa watu wamfanyie course work eti nae anaibuka kidedea.
Tagged:

Comments

  • @Vailethtz wewe ndio umesema, sometime hii hali inaboa sana, yaani wewe upo unakomaa na pepa mwingine hapo jirani ana jibia simu yaani kila hand out anayo, binafsi hili suala ata linafanya mwanafunzi adharau elimu, aone kumbe nayo ni magumashi tu, ni mbaya sana, na inakatisha tamaa kwa yule anayesoma kwa bidii.
Sign In or Register to comment.