Suala la mikopo ya elimu ya juu mchawi ni nani?

Jana wanafunzi wa chuo cha kodi, wamefanya maandamo ya amani, japokuwa wengine walipokuwa wanahojiwa walitia simanzi sana, machozi yaliwatoka na kuonesha hali ya kukata tamaa. Kuna moja aliongea jambo la msing sana, nitamnukuhu. Alisema " Inchi hii haiwezi kusonga mbele kama wanaosimamia kodi hawatakuwa wazalendo, sasa ni vizuri serikali itusomeshe kizalendo ili na sisi tuje tuwe wazalendo tutapoanza kufanya kazi". Kwa kweli huu ujumbe kama ni mwiba basi ni wa katani, maana ulichoma kwelikweli. Sasa bodi yetu ya mkopo (heslb) inasema tayari mikopo ipo vyuoni, ila vyuo navyo vimekuwa kimya na wanafunzi wengi hawajapa mikopo kama wizara ya elimu inavyosema, kuwa asilimia kubwa ya pesa za mikopo imeshatolewa. Sasa hapa mchawi ni nani? Na unadhani hatua ganizichukuliwe?

Comments

Sign In or Register to comment.