Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

Chuo cha CBE chafanya Mahafali ya 51, zaidi ya Wahitimu 1800 watunukiwa tuzo za kozi zao

edited November 2016 in Education

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) leo Novemba 12.2016, kimeweza kufanya Mahafali yake ya 51, Ambapo imewatunukia tuzo wahitimu wake katika kozi 20 huku jumla ya wahitimu wakiwa 1811 wakiwemo wanaume 886 ambao ni sawa na asilimia 48.9 (48.9%) na Wanawake 925 (51.1%) tuzo ambazo wametunukiwa na Mgeni rasmi Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ambaye aliwkilishwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage.

Katika Mahafali hayo yaliyojaa shamrashamra na hamasa kemkem kutoka kwa wahitimu pamoja na ndugu na jamaa yameweza kufahana kwa ustadi mkubwa na kipekee kwa namna yalivyoandaliwa ambapo wahitimu wote 1811 walipata wasaha wa kutunukiwa kwa heshima kubwa tuzo hizo za za kozi zao.

Awali mgeni rasmi Mh. Charles Mwijage wakati wa kusoma hotuba kwa wahitimu hao aliwaasa kuzingatia kile walichojifunza na kisha kukifanyia kazi ikiwemo uwezo wa kutumia maarifa waliyoyapata na kuyatumia hapa nchini huku akitumia nukuu ya neon ‘Bibi wa nyumbani’.

“Ujenzi wa uchumi wa viwanda unategemea sana viwanda vidogo sana, viwanda vidogo na viwanda vya kati. Asilimia 38 ya GDP ya India unategemea viwanda vidogo. Viwanda vidogo uzuri wake mtu yoyote anaweza kuanzisha. Hivyo njia ya kujiajili ni kuanzisha kiwanda kidogo hata kama umemaliza darasa la saba, Kinachotafutwa ni faida na wala musiwe na mapenzi na shughuli za uzuri wa ofsi uliyoajiliwa ama unafanyia kazi bali ni utashi wa faida ili kujituma katika shughuli zako” alieleza Waziri Muijage.

Amewahusia wahitimu hao kuhakikisha wanaanzisha kwanza biashara ndogo ili kumiliki biashara zao wenyewe kwa ngazi yoyote iwe mjini ama kijijini ambapo fursa za masoko ama namna ya ufanyaji biashara umehimalishwa.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha CBE, Prof. Emanuel Mjema ameeleza kuwa chuo anachokiongoza kimeendedelea kupata sifa ya kuwa chuo bora ndani na nje ya nchi kwa kuwa kimewatoa viongozi mahiri ambao waliotoa mchango katika maendeleo ya taifa.

Ameeleza kuwa CBE kilianzishwa mwaka 1965 kikiwa na wanafunzi 20 tu ili hali sasa kina wanafunzi zaidi ya 11,000 huku fani za elimu zikiongezeka kutoka ngazi ya cheti hadi shahada za Uzamili na masomo ya Uzamivu ambayo yanatolewa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Mashariki cha Finland.

“ Chuo chetu kimepiga hatua kubwa kimaendeleo toka kilipoanzishwa mwaka 1965, kimepata mabadiliko makubwa tumekuwa kitaaluma, kimachapisho na pia kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo fursa za biashara wakati huu ambao Serikali inahamia mkoani Dodoma” Amesisitiza.

Ameongeza kuwa chuo hicho kitaendelea kusimamia weledi katika utoaji wa elimu hapa nchini ili kiendelee kutoa vijana wenye weledi na uwezo wa kutekeleza majukumu mbalimbali kulingana na fani walizosomea.

“Chuo chetu tunasisitiza ubora wa elimu, tunafanya mchujo kwa kila mwaka ili kudhibiti ubora wa elimu yetu wale wasiofikia viwango kwa kila mwaka tunawaacha warudishwe nyuma sio kila anayeingia hapa lazima ahitimu masomo yake wale wasiokidhi viwango na kuendana na kasi ya masomo chuoni hapa wanajiondoa wenyewe” Amesisitiza Prof. Mjema.
Sign In or Register to comment.