Howdy, Stranger!

It looks like you're new here. If you want to get involved, click one of these buttons!

China kufadhili wanafunzi 120 wanaosomea lugha ya kichina kila mwaka

edited November 2016 in Education

Ushirikiano wa kiutamaduni baina ya nchi ya Tanzania na China unazidi kuimarika ambapo ubalozi wa China nchini umepanga kufadhili wanafunzi wa elimu ya juu 120 kila mwaka ambao wanakwenda kusomea tamaduni na lugha ya kichina nchini humo.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nuru Millao katika maonyesho ya kuenzi watunzi na waandishi wa tamthilia wa nchini China, ametoa wito kwa vijana kuitumia fursa hiyo ya kielimu.

“Vijana wengi wanakwenda China kujifunza lugha na tamaduni za kichina, hivyo natoa wito kwa wengine kuitumia fursa hii,” amesema.

Hata hivyo, Millao amesema hapa nchini pia elimu ya lugha ya kichina inatolewa katika vyuo vikuu vya Dodoma na Dar es Salaam, pamoja na shule za sekondari sita.

Balozi wa China nchini Zhu Yajing ameahidi kuwa serikali yake itaendeleza ushirikiano wa kiutamaduni hasa kwa kubadilishana elimu ya tamaduni na lugha za nchi hizo.

“Tuanatakiwa kuimarisha ushirikiano wetu hasa katika kubadilishana elimu ya tamaduni zetu, hapa Tanzania kuna sekondari zipatazo sita zinafundisha somo la elimu ya kichina na China nako kuna vyuo vikuu 4 vinafundisha kiswahili,” amesema.
Sign In or Register to comment.